WAZIRI UMMY AFAFANUA MADAKTARI BINGWA KUFANYA KLINIKI BINAFSI HOSPITALI ZA UMMA


 

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema utoaji wa huduma za afya kwa madaktari bingwa baada ya saa za kazi katika hospitali za umma sio jambo jipya huku akisisitiza lengo ni kutoa motisha kwa madaktari hao na kuboresha huduma za afya.


Waziri Ummy ametoa taarifa hiyo katika mitandao yake ya kijamii (Twitter na Instagram) leo Jumatano Julai 12, 2023.

“Utaratibu wa utoaji huduma za afya baada ya masaa ya kazi (Intramural Private Practice) sio mpya - Kwa Hospital kubwa kama Muhimbili una zaidi ya miaka 20, JKCI na MOI una zaidi ya miaka 15,”amesema.

Aidha, amesema katika kusimamia utaratibu huo, Ummy amesema kila hospitali inayotoa huduma hiyo inakuwa na miongozo maalumu ya utekelezaji iliyopitiwa na bodi ya hospitali husika.

Post a Comment

0 Comments