YANGA YAMTAMBULISHA KOCHA MSAIDIZI ALIYECHUKUA MIKOBA YA KAZE


Klabu ya Yanga katika kujiimarisha upya na msimu ujao imefanikiwa kumshusha Moussa Ndao kuwa Kocha Msaidizi akichukua nafasi ya Cedric Kaze
Dar es Salaam. Klabu ya Yanga imemtangaza Mousa Ndao raia wa Senegal kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo akisaidiana na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kuhakikisha wanatengeneza timu imara msimu wa 2023/2024.

Ndao (54) amewahi kuzifundisha timu za Wydad Athletic msimu wa 2014 mpaka 2016. Timu nyingine ni Sportive Jeanne d’Arc, Sporting Club Chabab Mohammed.

Kocha huyo aliyekuwa akicheza nafasi ya mshambuliaji katika timu ya taifa Senegal na vilabu kama Wydad Casablanca ya Morocco msimu wa mwaka 1991/1992, Al Hilal na Al Ittifaq zote za Saudi Arabia.

Vilevile Ndao anachukua nafasi ya Cedric Kaze ambaye alikuwa msaidizi wa Nasrredine Nabi katika msimu uliopita wa 2022/23 ambapo walifanikiwa kuandika historia ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza na kushindwa kunyakua taji hilo kwa bao la ugenini.

Post a Comment

0 Comments