KITAYOSCE NA FOUNTAIN GATE ZAFUNGIWA...!

 

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa Klabu za Kitayosce iliyoko Ligi Kuu ya NBC, na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship zimefungiwa kusajili wachezaji.


Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya Kocha Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hizo. Kocha huyo raia wa Misri ambaye alizifundisha timu hizo kwa nyakati tofauti alifungua kesi FIFA akipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu.

Baada ya Soliman kushinda kesi, klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini hazikutekeleza hukumu hizo.

Post a Comment

0 Comments