WANACHAMA WAKATAA KUIPA UKRAINE MUDA WA KUJIUNGA MKUTANO WA NATO


 

Mataifa ya Nato yamesema Ukraine inaweza kujunga na muungano huo wa Kijeshi , wakati wanachama watakubaliana na masharti kuafikiwa baada ya Zelensky kukosoa ucheleweshaji wa nchi yake kujiunga na Muungano huo.

Katika Taarifa yake , Nato ilisema inatambua umuhimu wa kuharakisha lakini haitatoa muda sahihi .

Mapema bwana Zelensky alisema kwamba inaonekana utayariya kuialika Ukraine kujiunga na Nato amba hata kuifanya kuwa mwanachama wa Muungano huo.

Hivi sasa yuko katika mji mkuu wa Lithuania Vilnius , ambapomkutano huo unafanyika.

Ukraine inakubali kwamba haiwezi kujiunga na Nato wakati ambapo ipo katika vita na Urusi lakini inataka kujiunga na Muungano huo mara moja vita vitakapoisha.

Lakini bwana Zelensky katika ujumbe wake wa Twitter alisema kwamba ukosefu wa muda sahihi wa kujiunga na Muungano huo kunamaanisha taifa lake huenda likajiunga na Muungano huo baada ya masharti kadhaa.

"Dirisha la fursa linaachwa ili kujadili uanachama wa Ukraine katika Nato katika mazungumzo na Urusi. kutokuwa na uhakika ni udhaifu," alisema.

Nato inaweza kuwa haijasema lini na jinsi Ukraine inaweza kujiunga na muungano huo. Lakini wanadiplomasia walisisitiza kwamba walikuwa wameweka njia wazi zaidi ya uanachama, na mchakato mgumu wa maombi umefupishwa kwa kiasi kikubwa.

Muungano huo ulikuwa umetambua kuwa jeshi la Ukraine lilikuwa linazidi "kushirikiana" na "kuunganishwa kisiasa" zaidi na vikosi vya Nato na ungeendelea kuunga mkono mageuzi ya sekta ya demokrasia na usalama ya Ukraine.

Post a Comment

0 Comments