TWAHA KIDUGU KUNYUKANA NA MBRAZIL


Bondia Twaha Kassim ‘Kiduku’ anatarajiwa kupanda ulingoni Julai 29, mwaka huu dhidi ya Bondia kutoka Brazil, Yamaguchi Falcao katika pambano lisilokuwa la ubingwa litakalopigwa jijini Mwanza.

Kiduku amesema pambano hilo litakuwa la raundi 10 katika uzito wa kilo 76 na tayari ameanza maandalizi kuelekea pambano hilo ambapo ameweka kambi nyumbani kwao, Morogoro.

“Sitawaangusha mashabiki wangu, naendelea na maandalizi mazuri ili kushinda pambano hilo ambalo limeandaliwa na Mo Green,” amesema bingwa huyo wa mkanda wa kimataifa wa UBO.

Kiduku alicheza pambano lake la mwisho la kimataifa Aprili mwaka huu dhidi ya bondia lago Kiziria kutoka Georgia na kushinda kwa alama tatu.

Mabondia wote wawili wana nyota mbili na ubora unaokaribiana hivyo ni kipimo kizuri kwa Kiduku kuendelea kujiimarisha kwa kulinda kiwango chake.

Post a Comment

0 Comments