LIGI YA WILAYA IRINGA IRINGA MJINI WANASUBIRIWA TFF TU


Katibu wa Chama cha mpira Manispaa ya Iringa (IRFA) Yahya Abdalah Mpelembwa amesema kuchelewa kutangazwa kwa ligi ya wilaya ndani ya Manispaa ya Iringa ni taratibu toka Shirikisho la soka Tanzania TFF.


Akizungumza na Shamba fm radio Mpelembwa amesema wao IRFA kila kitu kipo sawa wanachosubiri ni maelekezo toka TFF .

“Kila kitu kipo sawa na mdhamini Fredy Ngajilo (Vunja Bei) tunaye kwa mkataba wa miaka mitatu tunachosubiri ni kuona kama tunaungana na Iringa vijijini katika ligi moja ambao nao bado hawajatangaza” Amesema Mpelembwa

Ligi ya Wilaya Kilolo inatarajiwa kuanza Julai nane huku ligi ya Wilaya ya Mufindi pia ikianza Jumamosi chini ya udhamini wa Wabunge Justin Nyamoga wa Kilolo na Kosato Chumi wa Mafinga.

Nini maoni yako katika maagizo ya TFF ya kuwatumia wachezaji chini ya miaka 20 katika michuano hii??

Post a Comment

0 Comments