MAJI YATUMIKE KWA KIWANGO SAHIHI 

Wananchi wilayani Mufindi wameshauriwa kutumia maji kulingana na kiwango kinachotakiwa ili kulinda afya zao ikiwemo kuwa na kumbukumbu nzuri.


Wito huo umetolewa na afisa tabibu kutoka kituo cha afya DRH Kinyanambo Dkt. Elia Nyalusi wakati akizungumza na Mufindi Fm kuwa kunywa maji kwa kiwango sahihi kunasaidia kulinda mwili wa binadamu.

Aidha Dkt. Elia ameongeza kuwa kunywa maji kwa kiwango kilichopitiliza kunaweza kupelekea matatizo ya figo katika mwili wa mtumiaji wa maji hayo.

Nao baadhi ya wananchi kutoka wilayani Mufindi wamesema kuwa uelewa wao juu ya matumizi ya maji katika mwili wa binadamu ni kwa ajili ya kupuguza sumu mwilini.

Maji ni muhimu kwa binadamu ambapo asilimia 75 ya mwili wa binadamu ni maji na Kiwango cha mtu kunywa maji kwa siku ni kuanzia lita 1 hadi 4.

Post a Comment

0 Comments