UTAMBULISHO RASMI WA MESSI NI JULAI 16

 


INTER Miami imethibitisha itamtambulisha rasmi Lionel Messi, Julai 16 mbele ya mashabiki baada ya kukamilisha uhamisho wake akitokea Paris Saint-Germain. Messi atakaribishwa kuanzia saa 8:00 mchana na kutakuwa na burudani mbalimbali, vile vile atazungumza na mashabiki na mengine mengi kwa mujibu wa klabu hiyo.

.
Huenda Messi akatambulishwa pamoja na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona, Sergio Busquets na Jordi Alba. Vile vile Inter Miami ipo katika mkakati wa kumshawishi Eden Hazard ajiunge na klabu hiyo inayomilikiwa na David Beckham.

Post a Comment

0 Comments