BALEKE AWAAGA WANASIMBA " GOOD BAI "


 

JEAN OTHOS BALEKE amerejea nyumbani kwao nchini DR CONGO, Kubadilisha Pasi yake ya Kusafiria (PASPORT) ambayo imejaa tofauti na mashabiki wengi wa soka walivyodhani kuwa anaondoka Simba SC baada ya kupata timu nyingine.


Moja ya Kiongozi Simba SC akizungumza nami ameniambia Jean Baleke anarejea nyumbani kwao nchini DR. CONGO kubadilisha pasport yake ambayo imejaa na hivyo kumnyima nafasi ya kupatiwa VISA ya kuingia nchini Uturuki.

"Baleke hawezi kuondoka Simba SC ila tu anarejea nyumbani kwao kwenda kubadilisha PASPORT yake ambayo imejaa kwa hivyo amekosa Visa ya kuingia nchini Uturuki ila akishabadilisha Pasi yake ya Kusafiria na kupata Visa ataungana na wenzake ambao wataoondoka nchini Jumanne ya Julai 11." - amesema moja ya Kiongozi wa Simba SC.

Post a Comment

0 Comments