MABASI 38 YA NEW FORCE YASITISHIWA HUDUMA
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesitisha ratiba ya mabasi 38 ya New Force, kufuatia mfululizo wa ajali za mabasi hayo ambapo hadi sasa takribani mabasi matano ya kampuni hiyo yamepata ajali. 

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo amesema uchunguzi umeonesha kuwa, Madereva wake hawajathibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini.

Miongoni mwa ajali zilizotokea kupitia kampuni hiyo hivi karibuni ni ajali ya njombe katika eneo la Kijiji cha Igando wilayani Wanging'ombe  na kusababisha vifo vya watu saba papo hapo, na ajali iyotokea jana julai 02 katika eneo la mlima kitonga mkoani Iringa.

Post a Comment

0 Comments