MBUNGE FRANCIS MTEGA AFARIKI KWA AJALI YA PIKIPIKI

 


Mbunge wa Jimbo la Mbarali (CCM) Francis Leonard Mtega amefariki dunia leo tarehe Julai Mosi 2023, kwa ajali ya kugongwa na Trekta (Power Tiller) shambani kwake Mbarali, mkoani Mbeya.

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametangaza kifo cha Mtega leo na kutoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Jimbo la Mbarali.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Francis Leonard Mtega. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wa Jimbo la Mbarali. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika Tulia.

Post a Comment

0 Comments